Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia wachezaji wake watakaopewa nafasi kuitumia vizuri na kufanya kweli katika michuano ya Mapinduzi.
Yanga inaanza kazi leo kwa kukipiga na Mafunzo ya Zanzibar, mechi inayotarajiwa kuwa na mvuto kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Pluijm aliahidi kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa hawatumiki katika mechi za Ligi Kuu Bara ili wapate nafasi ya kuonyesha walichonacho.
“Hata hivyo kocha amewasisitiza ni lazima wafanye kweli, wacheze kwa juhudi na kuisaidia timu kwa kuwa Yanga iko Zanzibar kushiriki na kushinda na mwisho kubeba kombe,” kilieleza chanzo mara tu baada ya kikao cha Pluijm na wachezaji hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment