January 6, 2016


Ibrahim Ajib Migomba ameibuka shujaa wa Simba kwa mara nyingine baada ya kufunga bao pekee katika mechi dhidi ya URA kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Ajibu amefunga bao hilo kwa shuti kali katikati ya mabeki wa URA ya Uganda ambao hawakutegemea atapiga shuti katika mechi hiyo ya Kombe la Mapinduzi kutka Kundi B.

Kipindi cha kwanza, kilionekana kizuri kwa Simba, kwani pamoja na kupata bao lakini hawakutumia nafasi walizokuwa wakizipata.

Kipindi cha pili, walipoteza nafasi mbili  za wazi kupitia Dani Lyanga ambaye hakuwa makini katika umaliziaji.


Kwa ushindi huo, Simba ambao ni mabingwa watetezi wamefikisha pointi 4 huku wakisubiri mechi ya mwisho ambayo itakuwa dhidi ya JKU, Ijumaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic