January 13, 2016


Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema ameamua kukiimarisha kikosi chake kwa mazoezi zaidi ya stamina.

Azam FC wamefanya mazoezi mfululizo yakiwemo yale ya ufukweni na Stewart amesisitiza ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.

“Unapocheza mashinda, mfano Mapinduzi ukashinda au kutolewa, lazima utaona kuna upungufu wa jambo fulani. Benchi la ufundi kuna matatizo tuliyaona na tumeyafanyia kazi.


“Tunajua tunarejea Ligi Kuu Bara ambako kuna ugumu, lazima tujiandae vizuri zaidi. Ndiyo maana baada ya kutolewa Mapinduzi, nilisema tunaangalia mbele na ndicho tunachofanya sasa,” alisema Hall raia wa Uingereza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic