January 12, 2016


Kocha wa Simba, Dylan Kerr tayari yuko ndani ya boti akitokea Zanzibar kwenda jijini Dar es Salaam ambako atatimuliwa kazi.

Kerr ameitwa Dar es Salaam na uongozi wa Simba ambao unataka kumalizana naye ili mikoba yake akabidhiwe Mganda, Jackson Mayanja.

Mayanga amechukuliwa na Simba kama kocha msaidizi, lakini Simba ikaonyesha kiwango 'andazi' katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, jambo ambalo limeufanya uongozi wa Simba kushindwa kuvumilia.

Jana alipigiwa simu na mmoja wa viongozi wa juu wa Simba na kutakiwa leo kuja jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza kwamba yuko njiani akiwa na Kocha wa Makipa wa Simba, Iddi Salim ambaye pia taarifa zinasema naye atatimuliwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic