January 24, 2016


Baraka Deudeit ndiye atakuwa Katibu Mkuu wa Yanga wa muda kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka katika klabu hiyo.

Deudeit anachukua nafasi ya Dk Jonas Tiboroha aliyetakiwa kuchagua moja, kujiuzulu mwenyewe au afukuzwe kazi baada ya kubainika alificha barua za Haruna Niyonzima na kuidanganya kamati ya Nidhamu na ile ya Utendaji.


Taarifa zinaeleza, anayechukua nafasi ya Tiboroha ni kati ya waliokuwa wasaidizi wake lakini haijaelezwa kwamba mchakato wa kumpata katibu mkuu mpya utafanyika au Deudeit ambaye anajua mambo ndani ya Yanga yanaendaje, ataendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic