January 24, 2016

CHACHA (KUSHOTO) AKIWA NA MSEMAJI WA YANGA, JERRY MURO

Uongozi wa Yanga, umeamua kuachana na aliyekuwa mwanasheria wake, Frank Chacha.

Chacha alikuwa mkuu wa kitengo cha sheria cha Yanga. Taarifa zinasema kwamba uongozi huo umeamua kuachana naye.

Katika mkutano wa waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji unaondelea sasa hivi katika makao makuu ya klabu hiyo, Yanga sasa itachukua shughuli zake zote za kisheria kwa kuwakabidhi wanasheria nje ya klabu.


“Chache kama mkuu wa kitengo cha sheria klabuni, yeye tunamuacha aendelee na mambo yake na masuala yote ya kisheria, klabu itayafanya kutumia wanasheria, nje ya klabu,” imeeleza taarifa ya maandishi ya Manji kwa waandishi wa habari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic