January 18, 2016


Licha ya kuwa anatokea Uingereza, aliyekuwa Kocha wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, juzi Jumamosi alionyeshwa Jiji la Dar es Salaam lilivyo hatari, baada ya vibaka kumuibia simu yake na kumfanya ahangaike akiwasaka kila kona bila mafanikio.

Kerr ambaye bado yupo nchini akisubiri amalizane na Simba ili aondoke, alikumbwa na mkasa huo akiwa katika mitaa anayoishi, huko Kunduchi, Dar.

“Wajulishe watu kwamba simu yangu imeibiwa, vitu vyangu vingi muhimu vipo mule na sijui kama nitavipata, nawaomba walioiiba wairudishe tu,” alisema Kerr.

Hivi karibuni kocha huyo sambamba na yule wa makipa, Iddi Salim, walivunjiwa mikataba yao na Simba baada ya kuingia nao mkataba wa mwaka mmoja, Juni, mwaka jana.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic