Gwiji la Arsenal, Thierry Henry siku chache zilizopita amekutana na wakali wa michezo mingine na hii inaonyesha upendo ndani ya michezo.
Henry anayefanya kazi sasa katika runinga ya SKY, alikutana na bondia asiyepigika, Floyd Mayweather na baadaye gwiji wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu.
Watatu hao waliokuwa katika mechi ya mpira wa kikapu walionyesha furaha kubwa wakati wakisalimia baada ya mechi ya NBA kati ya LA Lakers na San Antonio Spurs.












0 COMMENTS:
Post a Comment