February 24, 2016



Timu ya mpira wa miguu ya wafanyakazi wa Global Publishers, Global FC, imetoshana nguvu na timu ya Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kaskazini, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Ijumaa iliyopita kwenye Uwanja wa Bora, Dar.

Timu zote mbili zilicheza kwa ustadi wa hali ya juu huku zikishambuliana kwa zamu lakini hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha kuashiria kumalizika kwa mchezo huo, hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake.

Nahodha wa Global FC, Philip Nkini, alisema kuwa mchezo huo ulikuwa ni moja ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea Mashindano ya NSSF yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.


“Mchezo ulikuwa mgumu kwani wapinzani wetu nao walijiandaa wakijua wazi kuwa wanakuja kukutana na timu ngumu, licha ya kutoka sare lakini timu yetu imeonekana kuimarika siku hadi siku, hiyo inatoa taswira kuwa tutafanya vizuri kwenye mashindano yajayo ambayo tunatarajia kwenda kushiriki,” alisema Nkini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic