February 21, 2016



Baada ya Azam FC kuitwanga Mbeya City kwa mabao 3-0 jana, Kocha Mkuu wa kikosi hicho kutoka Chamazi, Stewart Hall amesema bado wako kwenye nguvu za ubingwa.

Hall raia wa Uingereza amesema wana nafasi ya kuendelea kupigania ubingwa kwa kuwa wana kikosi bora.

“Katika mpira hauwezi kwenda moja kwa moja tu, ikitokea hivyo ujue ni mara chache sana. Lakini sisi bado tuko kwenye mbio za ubingwa.

“Wakati mwingine ni shida kidogo kwa kuwa ukiteleza kidogo watu wanakuwa na maneno hadi yanachanganya. Lakini hakukati tamaa,” alisema.

Azam FC imerejea katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 sawa na Simba iliyo katika nafasi tatu. Vinara sasa ni Yanga wakiwa na pointi 46.

Azam FC inaonekana kuwa na advantage zaidi kwa kuwa ina viporo vya mechi mbili ukilinganisha na Simba, kiporo cha mechi moja ukilinganisha na Yanga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic