February 20, 2016

CHUJI

Siku chache baada ya kutangazwa ametoweka kwenye kikosi cha Mwadui FC ya Shinyanga, kiungo Athumani Idd ‘Chuji’ amerejea kwenye timu hiyo inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Kiungo huyo, alitua kuichezea timu hiyo mwaka juzi wakati ikiwa Daraja la Kwanza na kufanikiwa kuipandisha Ligi Kuu Bara lakini msimu huu hakushiriki katika mechi nyingi.

Chuji amesema hakuwa kwenye kikosi hicho kutokana na maumivu ya kidole cha mguuni na alirejea Dar es Salaam kwa matibabu. 

 “Mengi yalizungumzwa wakati sipo na timu Shinyanga bila ya watu kujua sababu ya mimi kutokuwepo kambini na timu.


“Sikuwepo na timu kutokana na maumivu ya kidole cha mguu niliyoyapata nikiwa kambini na ilibidi nirejee Dar es Salaam kwa matibabu, nashukuru hivi sasa nimepona kabisa na nimeanza mazoezi na wenzangu,” alisema Chuji aliyewahi kuchezea Simba, Yanga na Taifa Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic