February 20, 2016


Nyingine kali hii hapa, maana vituko huwa haviishi katika mechi za watani kwani tayari mwamuzi Jonesia Rukyaa atakayechezesha mchezo wa leo wa Yanga na Simba amepewa majina ya wachezaji Juuko Murshid na Donald Ngoma.

Kisa cha Jonesia kupewa majina hayo ni tuhuma za utukutu wa Juuko wa Simba na Ngoma wa Yanga, hivyo kazi iliyobaki ni kuwatazama kwa muda mwingi wachezaji hao ‘wasiharibu’ mechi.

Taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Waamuzi Tanzania (Frat) zimedai kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kumuweka mwamuzi katika hali nzuri ya kutenda kazi yake.

 “Juuko anasifika kwa kucheza kibabe ikiwa ni pamoja na kufanya faulo nyingi za makusudi, kama vile kuwapiga viwiko wachezaji wenzake pasipo sababu yoyote.

“Ngoma yeye si mcheza faulo ila anasumbuliwa na hasira, amekuwa akivunja mara kwa mara taratibu, kanuni na sheria za soka kutokana na tatizo hilo, kila anapochezewa hujikuta akirudishia,” kilisema chanzo hicho.


Hii ni mechi ya pili ya Simba na Yanga ambayo Jonesia anaiamua baada ya ile ya kwanza ya Desemba 13, 2014 alipochezesha mchezo wa Nani Mtani Jembe ambapo Simba ilishinda 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic