February 12, 2016


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, ameweka wazi kuwa mmoja kati ya wachezaji watakaowahi kuondoka klabuni hapo na kufanikiwa zaidi kimataifa ni beki wa kushoto wa Wekundu hao, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Mayanja amesema hivyo baada ya kufanya kazi na mchezaji huyo kwa mara nyingine baada ya awali kuwa naye pamoja katika kikosi cha Kagera Sugar misimu miwili iliyopita.

MAYANJA

Aidha, Mayanja aliyechukua timu hiyo takriban mwezi mmoja uliopita akitokea Coastal Union ya Tanga, amesema kuwa moja ya silaha zitakazomfikisha mbali mchezaji huyo ni nidhamu ya soka aliyonayo.

Tshabalala ambaye ni mkimya, amekuwa akifanya kazi yake vizuri na kiwango kikionekana kupanda kila kukicha. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic