February 20, 2016



Simba imeanza na wageni wanne katika kikosi chake cha leo kinachowavaa wapinzani wake wakubwa Yanga ambao wao wameanza na wageni sita.

Katika kikosi chake cha kwanza, Simba imeanza na wageni hao wanne ambao ni kipa Vicent Agbani raia wa Ivory Coast, beki Juuko Murshid wa Uganda, kiungo Justice Majabvi pamoja na mshambuliaji Hamisi Kiiza.

Wakati Yanga wageni wake sita ni kuanza katika ulinzi, beki Vicent Bossou kutoka Togo, kiungo wa ulinzi Mbuyu Twite (Rwanda), kiungo mchezeshaji Thabani Kamusoko (Zimbabwe), kiungo wa pembeni Haruna Niyonzima (Rwanda) na washambuliaji Donald Ngoma (Zimbabwe) na Amissi Kiiza (Burundi).

Katika wachezaji wanne wa Simba, wanatokea katika mataifa matatu ya Zimbabwe, Uganda na Ivory Coast. Wakati yanga ni mataifa mataifa matatu tu ya Rwanda, Zimbabwe na Burundi.

Kwa hesabu zao, maana yake katika wachezaji 22 uwanjani kwa timu zote mbili kuna jumla ya wachezaji 10 watakaoanza mchezo wa leo ambayo ni 46% ya wachezaji walio uwanjani.

KIKOSI YANGA:
1. Ally Mustapha ‘Barthez’
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Pato Ngonyani
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Deus Kaseke
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Haruna Niyonzima

SUB
Deo Munish
Malimi Busungu
Nadir Harub
Geofrey Mwashiuya
Oscar joshua
Issofou Boubacar
Simon Msuva


KIKOSI SIMBA:
1. Vicent Agbani
2. Hassan Kessy
3. Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
4. Juuko Murshid 
5. Abdi Bhanda
6. Justuce Majabvi
7. Mwinyi Kazimoto
8. Jonas Mkude
9. Hamisi Kiiza
10. Ibrahim Ajibu
11. Said Ndemla

SUB:
Peter Manyika
Emry Nimubona
Lufungo
Awadh Juma
Dani Lyanga
Mussa Mgosi
Brian Majwega




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic