MPIRA UMEKWISHAAA
Dakika za mwisho Simba wanaendelea kucheza kwa ku relax wakionyesha wanasubiri filimbi ya mwisho
DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
GOOOOOOO Dk 88 Fully Maganga anaifungia Mgambo bao kwa shuti
SUB Dk 87 Simba wanamtoa Majabvi na nafasi yake inachukuliwa na Brian Majegwa
GOOOOOOO Dk 83 Kiiza anaifungia Simba bao la tano akiunganisha pasi safi ya Kessy
GOOOOOO Dk 77, Simba inapata bao la nne kupitia Lyanga aliyeingia muda mchache tu
SUB Dk 72, Simba inamuingiza Dani Lyanga kuchukua nafasi ya Ajib
Dk 66 hadi 70, Simba wanaendelea kucheza taratibu huku Mgambo wakionekana kukosa mipango wanaposonga kwenye lango la Simba
Dk 65, Kiiza anaruka kupiga kichwa mpira wa krosi wa Kessy, anashindwa kufunga
SUB Dk 62, Simba inamuingiza Ndemla kuchukua nafasi ya Hija Ugando
Dk 54 hadi 60, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja, huku Simba wakiupoozesha mchezo
Dk 53, Kazimoto anapiga shuti kali, lakini kipa Mgambo anadaka kwa ulaini
Dk 49 Agbani anafanya kazi ya ziada kuokoa inakuwa kona, mpira unapigwa, shuti la Zuri linaokolewa na kugonga mwamba
Dk 46 Simba wanapata faulo baada ya Ugando baada ya kufanyiwa faulo
MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 42 hadi 45, Simba wanaonekana kuridhika na mabao matatu kwa kipindi cha kwanza, wanacheza shoo zaidi
GOOOOOOO Dk 42 Ajib anaifungia bao la tatu, ilikuwa ni baada ya kuwachambua mabeki watatu wa Mgambo na kipa
Dk 35, Ajib anapiga mpira wa faulo, unagonga mwamba na kurudi uwanjani lakini Ugando anakuwa mzito kuokoa
GOOOOOO Dk 28 Kazimoto anaipatia Simba bao la pili kwa shuti kali baada ya kumtoka beki mmoja wa Mgambo
Dk 22 Mpaga wa Mgambo anapiga shuti kali kapiga, lakini mpira unatoka sentimeta chache tu
PENAAAAATTTTT Dk 14 Simba, wanapataka penalti, anakwenda kupiga Hamisi Kiiza lakini anafanya mashara na kumkabidhi mpira huo mikononi kipa Mudathiri ambaye anaudaka kwa ulaini kabisa
GOOOOOOO Dk 5, Hamisi Kiiza anaifungia Simba bao safi kabisa la kwanza
Dk 2, Kessy anaingia vizuri na kupiga krosi safi lakini Mgambo wanaokoa na kuwa kona, hata hivyo haina msaada
Dk 1, krosi safi kabisa inatua kichwani mwa Kiiza lakini anashindwa kulenga
0 COMMENTS:
Post a Comment