| MAYANJA... |
Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameamua kikosi chake kuwa kinapata dozi moja tu kwa siku.
Uamuzi huo wa Mayanja ni wakati wa maandalizi ya mwisho ya Simba kabla ya kuivaa Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa Jumamosi.
“Sasa tunafanya mazoezi mara moja tu kwa siku, kocha amepitisha hilo. Nafikiri kila tunavyokaribia mechi na ukali wa mazoezi unapungua,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba ambaye hataki kutajwa jina.
Simba imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mechi hiyo inayotarajia kuwa ngumu kwa kila upande.
Yanga ipo kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo pia na lengo kuu ni kuishinda Simba na kurejea kileleni.







0 COMMENTS:
Post a Comment