February 12, 2016

MAYANJA

Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja amesema anataka zaidi soka la kushambulia lakini kwa kasi.

Mayanja amesema wamekuwa wakiendelea kufanya mazoezi ya mambo kadhaa, lakini bado anahitaji muda.

“Mimi ninahitaji muda na vijana wanahitaji muda, ni kitu ambacho kipya kwa sasa.

“Lakini kila kitu kinawezekana, inategemea na mmejiandaa namna gani,” alisema Mayanja.

Simba inashuka dimbani kesho kuivaa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage jijini Dar es Salaam.

Tayari ipo mjini Shinyanga kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka mkoani Shinyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic