February 24, 2016


Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Davis Mosha alishaamua kuachana kabisa na masuala ya kwenda uwanjani kuangalia mechi.

Badala yake, Mosha ambaye ni mmoja wa aliyewahi kuwa viongozi vijana wa michezo nchini, amekuwa akiangalia mechi kwenye runinga tu.

“Mimi mara nyingi mechi naangalia kwenye tv, siendi uwanjani kabisa,” alisema Mosha.

Wiki iliyopita, Yanga ilikuwa na kibarua kigumu dhidi ya watani wake wa jadi Simba, lakini yeye aliendelea kuangalia kwenye runinga.

“Nina majukumu mengi yananibana, ndiyo maana nimeamua hivyo ingawa bado ninaendelea kufuatilia masuala ya soka hasa Yanga,” alisema Mosha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic