Lionel Messi ametoa pasi ya penalti kwa Luis Suarez naye hakufanya ajizi akapachika bao na kuifanya Barcelona kushinda mabao 6-1 dhidi ya Celta Vigo.
Bao hilo ilikuwa hivi, Messi alikwenda kupiga penalti, kama anapiga vile akaugusa kidogo tu ule mpira, Suarez akatoka nyuma kasi na kuumalizia wavuni kwa ulainiiii.
Kila sehemu ndiyo gumzo kwamba wawili hao wameingia katika rekodi kati ya wale waliowahi kupiga penalti ya pasi kama ile ya Thierry Henry na Robert Pires.
Ni haki yao,wapo duniani kwa Kazi mbili tu,Kumuabudu Muumba wetu na kutupia nyavuni basi,kama kuna mengine wanayoyafanya basi hayo ni ya ziada
ReplyDelete