February 6, 2016

KINNAH PHIRI
Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri amesema Mmalawi, Kinnah Phiri ataisaidia Mbeya City.

Phiri amesema anaamini kocha huyo Mmalawi ambaye ametua Mbeya City atakuwa msaada na changamoto kwa timu nyingi za Ligi Kuu Bara, kama ataungwa mkono.

“Phiri ni kocha mzoefu, anajua soka la ukanda wetu na Afrika kwa ujumla. Amefundisha Malawi na nje ya Malawi, kabla ya hapo amecheza ndani na nje ya nchi hiyo.
PATRICK PHIRI

“Anajua nini cha kufanya katika soka, kikubwa wamuunge mkono wakati anazoea mazingira,” alisema Phiri ambaye ni raia wa Zambia.


Mbeya City imeamua kuachana na kocha wake Mingange na kumchukua Phiri ili kuimarisha kikosi chake.

Lakini kabla ya hapo amezifundisha timu mbalimbali za Malawi pamoja na timu ya taifa ya nchi hiyo msaidizi wake akiwa ni Jack Chamangwana ambao wakati wa ujana wao, walicheza soka pamoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic