February 13, 2016


Mshambuliaji Mtanzania wa Genk, Mbwana Samatta ameanzia benchi kwa mara nyingine wakati timu yake ikiivaa Waasland-Beveren.

Kitendo hicho kinaonyesha kocha huyo amemwamini kwa mara nyingi, kwani kuna wachezaji wengi hawana hata nafasi ya kukaa benchi.

Mechi hiyo, Genk wako nyumbani na Samatta ni kati ya wachezaji walio benchi. Inachezwa usiku huu.

Inakuwa ni mechi ya pili anaanzia benchi. Katika mechi ya kwanza, Genk ilishindwa kwa bao 1-0 na Mtanzania huyo akaingia katika dakika 10 za mwisho.

Samatta amejiunga na timu hiyo akiwa na mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani akitokea TP Mazembe ya DR Congo aliyoisaidia kubeba ubingwa wa Afrika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic