February 10, 2016

TAMBWE

Straika wa Yanga, Amissi Tambwe, Jumapili iliyopita aliukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tambwe aliukosa mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kuisambaratisha JKT Ruvu mabao 4-0 kutokana na kuwa na kadi tatu za njano alizopewa katika mechi tatu tofauti zilizopita wakati akiitumikia klabu hiyo.

Hali hiyo ilimuumiza sana nyota huyo mwenye mabao 14 na kujikuta akisema: “Bahati yao JKT, ningefunga mabao mengi kwani ndoto zangu zilikuwa ni kuhakikisha naendeleza rekodi yangu ya hat trick hapa nchini.”

Tambwe amesema kuwa kabla ya mechi hiyo, alikuwa amejipanga vilivyo kuhakikisha anafanya maajabu mengine.
“Nilijisikia vibaya kwa sababu nilikuwa tayari nimeshajipanga kuhakikisha nafanya maajabu mengine katika mechi hiyo ili niweze kuendelea kuwa juu kwa kuzifumania nyavu.


“Hata hivyo, imeshatokea hivyo ngoja nijipange kwa ajili ya mechi nyingine kwani bado zipo nyingi kama Mungu atanijalia uzima na afya njema basi nitaendelea kufunga kwa sababu yeye ndiye anayejua kila kitu,” alisema Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic