February 25, 2016



Wachezaji wa Coastal Union wameamua kufunguka bila ya woga, sasa wanamuomba mdhamini wao wa zamani, Nassor Bin Slum, arejee kuokoa jahazi.

Bin Slum aliwahi kuwa mdhamini, aliyejitolea kwa hali na mali kabla ya kuamua kujiondoa kuepusha migogoro kutokana na chuki za baadhi ya viongozi.


Pamoja na wachezaji, baadhi ya mashabiki akiwemo kipa wa zamani wa Coastal Union, Shabani Kado wanaamini Bin Slum atakuwa msaada.

Lakini kupitia mitandao mbalimbali, wachezaji kadhaa wa Coastal Union ambao wamelalamika kutolipwa mishahara ya miezi mitatu, wamemuomba Bin Slum, kurejea.


Awali, leo wachezaji hao walipiga picha katika bango wakilalama kutolipwa fedha zao za mishahara ya miezi mitatu lakini pia posho na fedha zao nyingine.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic