February 10, 2016


Wanachama kadhaa wa klabu ya Simba wako mjini Shinyanga kuhakikisha kambi ya kikosi hicho iko salama, salimini.

Wanachama hao pamoja na wanachama wamekuwa wakiweka ulinzi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna figisu au ujanja nje ya uwanja.

Simba inatarajia kushuka dimbani Kambarage mjini Shinyanga, Jumamosi kuwavaa wenyeji wake Stand United.

Kwa kuwa Stand United ni timu ya wanachama, lazima figisu hazikosekani.

Wanachama wa Simba, hasa wale kutoka jijini Dar es Salaam, wanalijua hilo hivyo ambacho wamekuwa wakifanya ni kuhakikisha timu yao iko kwenye usalama

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema hiyo ni moja ya utamaduni wa Simba, wanachama wanahakikisha wapiganaji wao wako salama.

“Wako wanachama kutoka Dar es Salaam, wanashirikiana na wa hapa (Shinyanga). Lengo ni kuona vijana wako salama.

“Ukirudi upande wa wachezaji, kweli wanaendelea vizuri sana na mambo mengine yanaendelea katika mpangilio wake,” alisema Manara.


Simba imekuwa ikishinda mechi zake mfululizo hali iliyoamsha matumaini mapya na wanachama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic