February 19, 2016



Salaam wana Simba wenzangu,

Mwezi mmoja nyuma niliwahi kuwaambia waandishi tuulizane ubingwa baada ya mwezi wa nne mwaka huu na pia niliwaambia ubingwa uko wazi kwa yoyote na sisi Simba.tunayo nafasi kubwa ya kuwa mabingwa.

Wapo waliokebehi na wapo waliodhihaki kuna waastarabu waliguna. Yote ni kuonyesha kuwa ni ndoto kwa Simba kuchukua ubingwa!!

Leo hii kila mmoja anajua ubingwa wa ligi kuu upo wazi kwa yoyote yule huku tuliokuwa tukikebehiwa ndio tunaoongoza ligi.

Ubingwa wa ligi ni sawa na mbio za marathon.humjui mshindi hadi afike kwenye kamba.na sisi tunaamini msimu huu tutakuwa wa kwanza kugusa kamba.

Nimeanza na utangulizi huu maksudi kabisa kuwakumbusha washabiki wetu juu ya umuhimu wa kushinda kesho.ni mchezo tunaohitaji alama tatu na heshma ya klabu.

Kwa upande wetu kama viongozi tumehakikisha kila lihitajikalo kwa maana ya maandalizi limekamilika.
Na upande wa wanandinga wetu nao wapo vzuri kimwili na kiakili. Shughuli imebaki kwenu wapenzi wa mnyama.

Na shughuli yenyewe kwanza kuja uwanjani kwa wingi tena na jezi rasmi ya Simba.
Pili kushangilia timu muda wote na si kushangilia tu. Bali kuhanikiza kwa nguvu zote.


Tatu kwa wale ambao hawataajaliwa kuja taifa kesho.tunaomba dua na sala zenu. Kila mmoja kwa imani yake atuombee kwa mungu ushindi na salama. Sisi tunaamini hata ujiandae vp kama mungu hajaandika haiwi. Lakini pia tunaamini kudra ya mungu inazuiwa na dua tu.

Tunajua si wote mtakaojaaliwa kuja uwanjani ila tunaamini hakuna mwanasimba tutakaekosa dua na sala zake kwa kesho.

Mwisho niwataarifu kuwa kanuni znatutaka kama wageni tukae upande wa kulia kwenye benchi na vyumbani. Simba tutatii bila wasiwasi kanuni hyo na ni matarajio yetu, wenzetu hawatakuwa na woga wa kutekeleza kanuni hizo madhubuti za soka.

Niwatakie usiku mwema na niwatakie amani na salama kuelekea mchezo wa kesho.

Reclaiming our glory
Simba Nguvu Moja


Wa ukae Haji mwana wa S. Manara

1 COMMENTS:

  1. nikopamoja nawe manala nampila wa simba na yanga aautabiliki ila ushindi kwa simba auzuiliki labda yanga kama wameloga kwasabu ndo zao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic