February 19, 2016

WAZIRI NAPE

Mashabiki waliokosa tiketi na wale waliopata, wamemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuliingilia suala la mapato katika mchezo wa Yanga na Simba.

Yanga inaivaa Simba kesho katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki hao, walikuwa wakilalama baada ya kukosa tiketi. Lakini hata waliopata waliamini kuna wizi wa mapato ya fedha zinazopatikana.

“Unajua Simba au Yanga haziwezi kuiadhibu TFF, serikali iingilie na kusaidia katika hili kwa kuwa kuna wizi wa mapato.

“Waziri Nape ni mchapakazi, tunajua na tunaomba aingie na kulifanyia kazi hili tafadhari,” mashabiki hao walikuwa wakisema kwa jazba, tena kila mmoja akizungumza kwa wakati mmoja.

"Wakati wa Tenga, mapato yalionekana kuwa zaidi. Utaona mechi ya Simba na Yanga inaingiza hadi Sh milioni mia sita au mia tano. Siku hizi watu walewale lakini mapato ni Sh milioni mia mbili," alisema shabiki mwingine huku akishangiliwa na wenzake.


Mashabiki hao walilalamikia upatikanaji wa tiketi za Sh 7,000 wakidai zimefichwa ili kuwakomoa kwa kuwa baadaye watauziwa kwa bei ya juu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic