![]() |
| POULSEN AKIWA KAZINI WAKATI ALIPOKUWA AKIINOA TAIFA STARS... |
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amehoji uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuamua kumrejesha Kocha Kim Poulsen nchini.
| WAZIRI MKUU MAJALIWA |
Majaliwa amehoji wakati alipokutana na viongozi wa vyama vya michezo jijini Dar es Salaam, jana.
TFF ilichukua uamuzi wa kumfukuza Poulsen na kumlipa mamilioni ya fedha mara tu baada ya uongozi mpya chini ya Jamal Malinzi kuingia madarakani.
TFF ya Malinzi ilimuondoa Poulsen na nafasi yake kuchukuliwa na Martin Nooij raia wa Uholanzi ambaye sasa anashikilia rekodi ya kuboronga vibaya sana kuliko makocha wote wa kigeni kwa kipindi cha miaka 15.
Waziri Mkuu Majaliwa alionyesha kushangazwa na kuhoji kwa nini walimuondoa na imekuwaje wanamrejesha.
“Kwa nini aliondolewa, sasa kwa nini sasa anarejeshwa. Tafca ndiyo walipaswa kukagua vyeti kwa ajili ya uhakiki, lakini ndiyo mmevunja ofisi zao,” alisema Majaliwa akipinga uamuzi wa TFF kuvunja ofisi za Chama cha Makocha Tanzania (Tafca).








0 COMMENTS:
Post a Comment