February 18, 2016



Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesisitiza kuanza tena matumizi ya tiketi za elektroniki.

Majaliwa ameyasema hayo baada ya kukutana na viongozi wa vyama vya michezo jijini Dar es Salaam, jana.

Majaliwa ametaka mechi zote za soka baada ya kesho dhidi ya Yanga na Simba, kuanza kutumia mfumo huo.

Awali ulianza, lakini ukaonekana kuna migongano mingi huku ikionyesha wazi kuna watu wakiwemo kutoka TFF hawakuwa wakitaka utumike kwa kuwa hakukuwa na juhudi za dhati kukuhakikisha mfumo huo unatumika.


“Lazima tiketi za elektroniki zianze kutumika, mfumo huo utasaidia kudhibiti ubadhirifui wa mapato,” alisema waziri mkuu wakati akisisitiza hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic