HILI ni bonge la bahati aisee! Wapenzi wa soka hapa nchini wamepata fursa ya kwenda nchini Hispania kushuhudia mechi kati ya Barcelona yenye nyota kama Lionel Messi na Neymar ambayo itapambana na Deportivo la Coruna, April 17, mwaka huu.
Fursa hiyo imetolewa leo hii na Azam Media kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo baada ya kutangaza ushirikianao wao juu ya mpango huo ambao utawapa nasafi hiyo watumiaji wa huduma za Tigo Pesa wanaonunua vifurushi vya michezo vya Azam TV.
| BOSI WA MASOKO AZAM MEDIA, MGOPE KIWANGA |
Mkuu wa Masoko wa Azam Media, Mgope Kiwanga na Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta wamesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa Watanzania wengi wana mapenzi makubwa na soka hasa Ligi Kuu ya Hispania.
“Kutokana na hali hiyo ndiyo maana tumeamua kuungana na Azam Media pamoja na Liga BBVA ili kutoa nafasi kwa Watanzania kwenda kushuhudia mechi hiyo kati ya Barcelona na Deportivo la Coruna nchini Hispania," alisema Mgope.
| MENEJA WA PROMOSHENI WA TIGO, MART RUTA |
“Ili kupata nafasi hiyo ya kwenda kuzishuhudia timu hizo, mtumiaji wa Tigo Pesa anatakiwa kuhakikisha kifurushi kimoja kati ya vifurushi vya Azam TV kipo hewani na hapo atakuwa ameingia katika droo ya kumpata mshindi wa kwenda kushuhudia mechi hiyo ikiwa ni pamoja na kupiga picha na Messi pamoja na Neymar,” alisema Marry.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kuichangamkia nafasi hiyo kwani haijitokezi kila mara kushuhudia maajabu ya Messi na Neymar yakitokea uwanjani.
“Mbali na washindi wawili watakaosafiri kwenda Hispania pia katika promosheni hiyo kutatolewa zawadi mbalimbali kwa wasindi wengine kama vile mipira, jezi, tisheti, kalamu, miwani ya jua na nyingine nyingi,” alisema Torrington.
Azam TV ilikuwa ni chaneli ya kwanza ya televisheni kuanza kuonyesha La Liga kwa lugha ya Kiswahili.
Kupitia La Liga na Ligi Kuu Bara, Azam TV imekuwa ikijipatia umaarufu mkubwa na kupata idadi kubwa ya watazamaji.
| CHARLZ HILARY |
| MVULA NA KILUMANGA.... |
| WADAU MUHIMU NAO WALIKUWEPO... |







0 COMMENTS:
Post a Comment