Na Mwandishi Wetu, Pemba
Yanga inatarajiwa kuwasili leo jijini Dar ikitokea Pemba ambapo imeweka kambi kwa takriban wiki moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.
Taarifa zinaeleza kuwa msafara huo wenye wachezaji 24 na viongozi sita, utaondoka kwa ndege maalum ya kukodi muda wa mchana, hii leo Ijumaa.
Katika mazoezi ambayo wamekuwa wakifanya kisiwani hapa, Yanga wamekuwa wakibadili ratiba lakini siku mbili zilizopita, walifanya mazoezi jioni.
Yanga iliweka kambi visiwani hapa kujiandaa na mechi yao dhidi ya Simba, kesho. Mechi hiyo iansubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini na nchi jirani.








0 COMMENTS:
Post a Comment