| YANGA WAKIPIGA TIZI KWENYE UWANJA WA GOMBANI |
Na Mwandishi Wetu, Pemba
Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Gombani mjini hapa.
Kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania kimeweka kambi mjini hapa kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, keshokutwa Jumamosi.
Yanga iliwasili muda wa kama saa 10 hivi jioni na kufanya mazoezi ahadi saa 12 na nusu jioni.
Kocha Hans van der Pluijm amesema hayo ndiyo mazoezi ya mwisho kisiwani hapa.
Yanga inatarajia kuondoka kesho mchana kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kambi ya siku moja kabla ya mechi dhidi ya Simba.







0 COMMENTS:
Post a Comment