March 2, 2016




APR imeonyesha inaichukulia kwa uzito mkubwa mechi dhidi ya Yanga kwa kuamua kuajiri kocha mpya raia wa Tunisia.

Nizar Khanfir aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Tunisia, anatarajia kutua nchini Rwanda ndani ya siku mbili hizi kuanza kazi ya kuinoa APR.

Kocha huyo wa zamani wa Stade Gabasien anatua Kigali wakati APR ikijiandaa kupambana na Yanga wiki moja ijayo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Ingawa viongozi wa APR wamekuwa wakifanya siri kubwa lakini Kanfir anaingia kwenye rekodi kwa kuwa kocha wa kwanza Mwarabu kufundisha soka nchini humo.


Kanfir pia amewahi kuzinoa timu zote kubwa tatu za Tunisia ambazo ni Club African, Esperance na Sfaxien.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic