March 2, 2016


Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Zimbabwe, inatarajiwa kuwasili kesho Alhamisi mchana wakiwa na msafara wa watu 29, wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Thabani Kamusoko ni raia wa Zimbabwe na kati ya viungo walio vizuri wa kigeni wanaokipa hapa nyumbani. Dada zake nao nao wako tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Twiga Stars.

Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.

Upande wa waamuzi wa mchezo huo wanatrajiwa kuwasili kesho mchana kwa shirikia la ndege la Kenya (KQ) wakitokea nchini Ethiopia, huku kamisaa wa mchezo kutoka Congo DR akiwasili jioni kwa KQ.

Maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, tiketi za mchezo huo zitauzwa eneo la uwanja Chamazi siku ya Ijumaa. Viingilio vya mchezo ni shilingi elfu mbili (2,000) kwa mzunguko na shilingi elfu tatu (3,000) kwa jukwaa kuu.


TFF inawaomba wadau, wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic