March 24, 2016Hatimaye Bodi ya Ligi (TPLB) inayosimamia ligi za soka nchini imefanya mabadiliko katika ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ratiba inayozingatia usawa, haki na inayopunguza kwa sehemu kubwa mnyukano wa viporo uliolundikwa pasi na sababu kwa klabu za Yanga na Azam.

Tunaamini mabadiliko hayo yatarudisha walau imani ilioanza kupotea kwa bodi na TFF toka kwa wapenzi, mashabiki na wanachama wa Simba.

Hakika viporo vile vilikuwa na taswira isiyopendeza kwa afya ya ligi na mchezo wenyewe wa soka nchini.

Sasa kwa spirit ile ile ya bodi na uharaka ule ule tunaamini TFF nao watashughulikia malalamiko mengine tuliowasilishia kwao.

Tunachokitaka kwa wakubwa hawa sio kupendelewa bali kupewa haki na sio kwa Simba tu, pia kwa klabu nyingine zote nchini.

Nawaomba wanachama na washabiki wetu mtuunge mkono katika mapambano haya mazito tunayoendelea nayo.

Mwisho kwa niaba ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, wajumbe wa kamati ya utendaji, sekretarieti, benchi la ufundi na wachezaji, tunawatakia furaha na baraka tele kuelekea kwenye sikukuu za Ijumaa Kuu na Pasaka.

Tunawapenda sana.

Simba Nguvu Moja

De la boss
Haji Manara


5 COMMENTS:

 1. Huyu zungu anatatizo katika ubongo wake

  ReplyDelete
 2. Haya ratiba imebadilishwa sasa imetoka ratiba ambayo inaziadhibu Yanga na Azam kwa kosa la kushiriki mashindano ya kimataifa na kutoa wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa.Hii hofu ya kupanga matokeo inatoka wapi?Huku sio kuzidharau timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu?Au ndio Simba wamezoea kupanga matokeo sasa wanadhani na timu nyingine ziko hivyo?Bodi ya Ligi hawajazitendea haki Yanga na Azam na sasa wasubiri malalamiko mengine pale Simba itakapokosa ubingwa na kuanza kulalamika kwa nini refa alikuwa mwanamke

  ReplyDelete
 3. Hofu imetokea kutokana na timu kuwa na viporo vingi kuelekea mwisho wa ligi huku vikigombea ubingwa wakati hakukuwa na sababu ya kutocheza katikati ya wiki kisha kusubiri mechi ya kimataifa mwisho wa wiki. Wenzetu walioendelea hawarundiki viporo kwa kisingizio cha kucheza michuano ya kimataifa.

  ReplyDelete
 4. Hofu imetokea kutokana na timu kuwa na viporo vingi kuelekea mwisho wa ligi huku vikigombea ubingwa wakati hakukuwa na sababu ya kutocheza katikati ya wiki kisha kusubiri mechi ya kimataifa mwisho wa wiki. Wenzetu walioendelea hawarundiki viporo kwa kisingizio cha kucheza michuano ya kimataifa.

  ReplyDelete
 5. Hofu imetokea kutokana na timu kuwa na viporo vingi kuelekea mwisho wa ligi huku vikigombea ubingwa wakati hakukuwa na sababu ya kutocheza katikati ya wiki kisha kusubiri mechi ya kimataifa mwisho wa wiki. Wenzetu walioendelea hawarundiki viporo kwa kisingizio cha kucheza michuano ya kimataifa.

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV