March 24, 2016


Taarifa kutoka katika magazeti mbalimbali ya Ulaya zinaeleza kwamba Cristiano Ronaldo anatarajia kupata mtoto wa pili.

Kitendo cha Ronaldo kuweka mpira tumboni baada ya kufunga bao, ndiyo kimeamsha jambo hilo.

Vyombo mbalimbali vya habari nchini Hispania, vimeeleza kwamba tayari Ronaldo amemtundika mimba mwanamke mmoja.

Mtoto wake wa kwanza, mambo yalikwenda kwa kificho hadi ilipojulikana baada ya Ronaldo mwenyewe kutangaza.

Ronaldo alisema ameingia mkataba na mtoto wa mama kwamba ataendelea kuwa “kimya” bila kujitangaza kwa muda wote na hayo ni makubaliano ya kisheria.


Hata hivyo, Ronaldo bado hajazungumzia lolote kuhusiana na mtoto wa pili kama ni kweli au la.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV