![]() |
| INFANTINO |
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.
Katika barua hiyo, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.
BARUA YAKE KWA INFANTINO HII HAPA...









0 COMMENTS:
Post a Comment