Kiungo myumbulikaji wa Simba, Ibrahim Ajib amefunguka kuwa licha ya kucheza kwa kujituma lakini amekuwa akipata wakati mgumu uwanjani pamoja na Mganda, Hamisi Kiiza kutokana na mara nyingi kucheza kwa kukamiwa na mabeki wa timu.
Ajib ambaye kwa sasa amekuwa miongoni mwa mastraika wanaochungwa uwanjani kutokana na kasi yake kupanda kwa kiwango cha juu, wikiendi iliyopita aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City.
Ajib alisema licha ya kucheza kwa kujituma uwanjani lakini changamoto kubwa inayomkabili kwa sasa ni kucheza kwa kukakimiwa na wapizani wao hali inayofanya abadili uamuzi.
“Ligi ilipofika imezidi kuwa ngumu licha ya kuwa tunapambana na kufanya vizuri katika michezo yetu kwa kuhakikisha tunatimiza malengo tuliyojiwekea msimu huu.
“Lakini changamoto ipo kwa wachezaji wa timu tunazokutana nazo wamekuwa wakicheza kwa kutukamia hasa mimi na Kiiza, yaani mchezaji atakavyocheza na timu nyingine anakuwa tofauti atakapokuwa na sisi hali inayolazimu wakati mwingine kufanya uamuzi ambao haukutarajiwa ila kimsingi tutaendelea kupambana nao katika kila mchezo na tupate matokeo mazuri,” alisema Ajib.
0 COMMENTS:
Post a Comment