Arsenal imebakiza mechi 11 ambazo dakika 990 zitakazoamua kama inaweza kuwa bingwa wa Premier League au La.
Timu nyingine zinazoonekana kuwa na nafasi kubwa ni Leicester, Tottenham na Man City ingawa bado si wakati mwafaka kuibeza Man United.
Kikosi hicho chini ya Arsene Wenger kinataka kukata kiu ya mataji ya Premier League. Lakini lazima kicheze vema karata hizo 11.
Kwa sasa Arsenal iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51, wakati vinara ni Leicester City wenye pointi 56 na Tottenham wako nafasi ya pili wakiwa na pointi 54.
Katika mechi hizo 11, sita ni za nyumbani ikiwemo ya kesho dhidi ya Swansea City. Ugenini ni mechi tano, mbili ni dhidi ya Tottenham na Man City ambayo pia zinaufukuzia ubingwa huo kwa udi na uvumba.
MECHI 11:
Machi 2 Swansea City (Nyumbani)
Machi 5 Tottenham Hotspur (Ugenini)
Machi 12 West Bromwich Albion (Nyumbani)
Machi 19 Everton (Ugenini)
Aprili 2 Watford (Nyumbani)
Aprili 9 West Ham United (Ugenini)
Aprili 17 Crystal Palace (Nyumbani)
Aprili 24 Sunderland (Ugenini)
Aprili 30 Norwich City (Nyumbani)
Mei 7 Manchester City (Ugenini)
Mei 15 Aston Villa (Nyumbani)









0 COMMENTS:
Post a Comment