March 25, 2016


Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wanatarajiwa kuivaa na Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini wakati mechi hiyo ikitarajiwa kuwa ngumu na maandalizi yakiendelea kwa pande zote, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ameweka wazi kuwa anawajua vizuri Waarabu hao. 

Mayanja alisema hayo wakati alipoulizwa juu ya mchezo huo wa wapinzani wao wa jadi, ambapo alisema Yanga itarajie kukutana na mlima mgumu kwa kuwa Al Ahly haina utani inapokuwa kazini, akidai kuwa anijua vizuri timu huyo ya Misri.

Mayanja ambaye pia aliwahi kuitumikia timu ya Al Masry ya Misri, ambayo ni wapinzani wakubwa wa Al Ahly alisisitiza kuwa Waarabu hao wanaonekana kujipanga na ndiyo maana anaamini mchezo huo utakuwa mgumu.

“Timu za Kiarabu mara nyingi zimekuwa zikitushinda sisi wa huku kutokana na umakini mdogo, wachezaji wao huwa na nidhamu ya hali ya juu ndani ya uwanja, lakini pia nje ya uwanja ambako wanaishi kwa kuzingatia taratibu za soka.

“Wachezaji wao wanazingatia sana maelekezo ya kiufundi wanayopewa jambo ambalo wachezaji wetu wa ukanda huu wa Afrika Mashariki hawana, wakichanganywa kidogo tu wanakubali matokeo na mwisho wa siku hupoteana uwanjani.

“Sisemi kwa nia mbaya ila ni kwa nia nzuri kwa Yanga sababu ni timu yetu, inanibidi nitoe maoni yangu kuhusiana na Al Ahly ambayo naijua vizuri kwa sababu wakati nacheza soka nilikuwa nikikumbana nayo mara kwa mara,” alisema Mayanja na kuongeza:

“Wito wangu kwa Yanga na kwa Azam FC pia ambayo itacheza na Esperance de Tunis ya Tunisia ambayo pia niliwahi kuitumikia nikiwa mchezaji miaka ya 1990 ni kwamba, kama timu hizo zinataka kushinda mechi zao basi kuanzia sasa zihakikishe zinawajenga wachezaji wao kuwa na nidhamu ya hali ya juu ya kimchezo na watumie muda huu kujiweka fiti.”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic