March 23, 2016




Pamoja ushindi wa mabao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Chad, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema ilikuwa mechi ngumu sana.

Mkwasa amesema vijana wake wamejituma vilivyo hadi kupata ushindi huo kwa kuwa walicheza katika mazingira magumu.

Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka ND'jamena, Mkwasa amesema ilikuwa ngumu sana hasa kutokana na hali ya hewa.

"Hali ya hewa ilikuwa mbaya kabisa lakini vijana wangu walijituma na wanastahili pongezi kabisa," alisema.

"Kipindi cha pili walitushambulia sana, lakini ilikuwa ni lazima kufanya hivyo ili kuhakikisha tunajilinda kuhakikisha hawasawazishi."
Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini.

Stars sasa imefikisha pointi 4 baada ya kucheza mechi tatu, ikiwa imepoteza moja, sare moja na kushinda moja.



Inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu katika Kundi H, Misri inangoza ikiwa na pointi 6. Nigeria ina pointi 4 sawa na Tanzania lakini kuna tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa na Misri na Nigeria zinakutana kukamilisha mchezo wa tatu pia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic