Gumzo la jiji la
Kigali ni Yanga dhidi ya wenyeji APR ambao wanajua wanakutana na timu yenye
safu kali ya ushambulizi.
Yanga itakwenda
Kigali kucheza mechi yake ya kwanza ya hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa
Afrika dhidi ya APR.
Lakini mashabiki wa soka jijini Kigali, Rwanda, tayari wanaamini Mtanzania, Mrundi na Mzimbabwe ndiyo hatari kwao katika mechi hiyo ya Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Amahoro.
Simon Msuva, Amissi
Tambwe na Donald Ngoma wamepewa jina la MTN, usifikiri ni ile kampuni kubwa ya
simu nchini humo badala ni kifupi cha majina yao ya ukoo.
Mashabiki wengi wa
mji wa Kigali ambao ni mkubwa kuliko yote Kigali, wanaamini washambuliaji hao
watatu watakuwa tatizo katika safu ya ushambulizi ya APR.
APR imevuka kwa
kuing’oa Mbabane ya Swaziland kwa jumla ya mabao 4-1 wakati Yanga imeondoa
Cercle de Joachim ya Mauritius.
0 COMMENTS:
Post a Comment