Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia waandishi wa habari jijini Kigali kwamba wanachotaka ni ushindi dhidi ya APR.
Pluijm raia wa Uholanzi, yuko mjini Kigali kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya APR ya Rwanda.
Mara baada ya Yanga kuwasili, waandishi wa habari walimzunguka kocha huyo na kutaka kujua ana lipi la kuzungumza.
“Tunataka kushinda na hicho ndicho kilichotuleta. Lakini tunajua APR ni timu nzuri, tunaheshimu hilo. Lakini hakika tunataka kutengeneza mazingira bora ya mechi ya marudiano kule Dar es Salaam.
“Kushinda huku (Kigali), kutafanya tuwe katika nafasi nzuri ya kufanya vema zaidi,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment