April 8, 2016


RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri klabu za Azam FC na Young Africans ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa itayochezwa wikiendi hii.

TFF imevitaka vilabu hivyo kupambana katika michezo inayowakabili na kuweza kufanya vizuri kwa kupata ushindi, ili kutengeneza mazingira mazuri katika michezo ya marudaino itakayochezwa Aprili 19-20 mwaka huu.

Young Africans wanaochezwa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afria (CAF CL) watashuka dimbani kesho Jumamosi uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki, kucheza dhidi ya Al Ahly katika mchezo namba 89 wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL).

Mchezo huo utachezeshwa na Dennis Dembele, akisaidiwa na Marius Donatien, Moussa Bayere, mwamuzi wa akiba Tangba Kambou wote kutoka nchini Ivory Coast, huku kamisaa wa mchezo huo akiwa Celestin Ntangungira kutoka nchini Rwanda.

Jumapili katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi saa 9 kamili alasiri, Azam FC watwakua wenyeji wa Esperance Sportive de Tunis (EST) ya Tunisa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) hatua ya 16 bora.


Waamuzi wa mchezo huo namba 75 ni Daniel Frazer Bennet, akisaidiwa na Zakhele Siwela, Thembisile Theophilus, mwamuzi wa akiba Mbongiseni Fakudze wote kutoka nchini Afrika Kusini, huku kamisaa wa mchezo akiwani Joseph Nkole kutoka nchini Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic