May 22, 2016

Timu nyingine ya Tanga, African Sports imeteremka daraja na kufanya timu mbili za mkoa wa Tanga kuwa zimeteremka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi daraja la kwanza.

African Sports imepigwa mabao 2-0 na wenyeji wao Mtibwa Sugar hivyo kubaki na pointi 26 zinazowafanya wabaki katika nafasi ya 15 katika timu 16.

Tayari Coastal Union ilishateremka daraja na kuwa timu ya kwanza katika ligi hiyo kuteremka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV