May 22, 2016

MAYANJA
Uongozi wa Simba, umeanza kazi kimyakimya ya kufanya mazungumzo na makocha kadhaa wa nje ya Tanzania.

Taarifa zinaeleza, uongozi wa Simba unataka kuimarisha benchi lake la ufundi kwa kusajili makocha wenye uwezo wa juu.

“Kweli hiyo kazi imeanza, lakini hatuwezi kusema ni kutoka wapi na itakuwaje,” kilieleza chanzo.

Taarifa nyingine zinaeleza kwamba Simba imeanza maandalizi pia ya kumpata kocha mpya wa makipa.

“Ninavyojua viongozi wa Simba wameamua kufanya mambo yao kimyakimya kwanza. Wanachunguza lakini watakachofanya kikubwa ni kuboresha benchi la ufundi.”


Kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda, alijiunga na Simba katika nafasi ya kocha msaidizi lakini kabla ya kuanza kazi, aliyekuwa Kocha Mkuu, Dylan Kerr akatimuliwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV