KINYOGORI WAKATI WA UHAI WAKE.... |
Askari Polisi wa Usalama Barabarani, Ally Kinyogori aliyeuwawa na watu wasiojulikana, aliaga kutokwenda kazini ili akaipokee Yanga Ijumaa.
Yanga ilikuwa inarejea nchini juzi Ijumaa ikitokea Angola ambako ilifanikiwa kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuing'oa Esperanca.
Kinyogori alitaka kwenda kuipokea Yanga, timu anayoipenda kuliko zote duniani.
....MARA KWA MARA ALIKUWA AKIJITOKEZA KUFUATILIA MAZOEZI YA YANGA. |
Mmoja wa askari anayefanya naye kazi, alisema Kinyogori alimuaga mapema kabisa.
“Alisema asingependa tumlaumu wakati tunajua Yanga inarejea, ilikuwa ni lazima awepo airport.
“Lakini kifo, hauwezi kujua. Haikuipata nafasi hiyo,” alisema rafiki yake ambaye hatutamtaja kwa kuwa si msemaji wa familia wala Jeshi la Polisi Tanzania.
Kinyogori aliuwawa baada ya watu wawili wenye silaha kuingia nyumbani kwake na kumpiga risasi tatu zilizochukua uhai wake.
Zaidi ya watu 10, akiwemo mke wake ambaye inaelezwa hakuwa katika uhusiano mzuri na mumewe wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Tanzania ambalo linaendelea na uchunguzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment