May 22, 2016


Ikiwa ni Ligi Kuu Bara inafikia ukingoni leo, nahodha wa Toto Africa, Hassan Khatibu ameamua kuachana na ukapera.

Khatibu amefunga ndoa jijini Dar es Salaam, juzi na sasa ni kiongozi wa familia.

Beki huyo wa kulia, amechipukia kisoka na kukulia chini ya klabu ya Simba.


Lakini sasa ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa kikosi cha Toto Africa ya Mwanza.

SALEHJEMBE INATOA HONGERA KWA KHATIBU NA KUMTAKIA UVUMILIVU NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YA NDOA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic