TIMU ya Azam FC, imepokwa pointi tatu na mabao matatu kutokana na kumtumia beki wao, Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam ilimchezesha Nyoni kinyume na sheria huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Azam wamepoteza mchezo ule na sasa Mbeya City imepewa pointi tatu na mabao matatu pia tumelipa onyo benchi la ufundi la Azam kuwa makini ili jambo hili lisiwatokee tena,” alisema Lucas.
0 COMMENTS:
Post a Comment