May 17, 2016


Rais wa Simba, Evans Aveva ametangaza Mkutano Mkuu wa timu hiyo kufanyika Julai 10, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hiyo ni siku chache tangu wanachama wa timu hiyo kuvamia kwenye Makao Makuu ya timu hiyo yaliyopo Msimbazi jijini Dar es Salaam wakishinikiza uongozi kuitisha mkutano.

Akizungumza na Salehjembe, Aveva alisema katika mkutano mambo mengi yatajadiliwa ya klabu hiyo kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyoyafikia ikiwemo kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Aveva alisema, taratibu zitakazofanyika ni zilezile zilizozoeleka katika kipindi chote cha mikutano yao ikiwemo kupokea baadhi ya agenda kutoka kwenye matawi yao.

“Uongozi ulikutana na kukubaliana baadhi ya mambo ikiwemo kuitisha Mkuu wa Simba tutakaoufanya Julai 10, mwaka huu,”alisema Aveva.


Wanachama wa Simba ndiyo wamekuwa wakisisitiza kufanyika kwa mkutano huo wakionyesha kutoridhika na mwenendo wa timu yao hasa katika hatua za mwisho kwenye Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV