Kocha wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja amesema Yanga imepata jembe baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Juma Mahadh kutokana na yeye kufahamu kiwango cha mchezaji huyo ambaye aliwahi kumfundisha kabla ya kuhamia Simba.
Mahadh ambaye ameonyesha kiwango kikubwa kwa msimu huu akiwa na Coastal Union kiasi cha kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars, amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mayanja ambaye ameiongoza Simba kumaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara amesema kuwa kutokana na kufahamu kipaji alichonacho kiungo huyo ana uhakika mkubwa ataisaidia Yanga msimu ujao.
“Mimi ndiye niliyemfanya Mahadh ajulikane kwani nilimkuta mtaani tu anacheza lakini kwa uwezo aliokuwa nao ndiyo nikamvuta Coastal Union ambapo ameonyesha uwezo wa hali ya juu mpaka sasa kusajiliwa na Yanga, jambo ambalo kwangu najisikia furaha kuona linatokea.
“Naamini kwamba Yanga wamepata mchezaji sahihi, atawasaidia sana kwa msimu ujao kwani uwezo anao na anaweza kuwapa changamoto viungo wengine aliowakuta kikosini,” alisema Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment